Historia ya Tanzania ilianza na wakoloni wa Ulaya. Karne ya 18 ilikuwa na dola ndogo za miji katika mwambao baada ya kukaliwa na waarabu kutoka Oman. Ilikuwa karne 7 baadae mwaka 1499 wakati baharia wa Kireno Vasco da Gama alipotembela visiwa vya Zanzibar. Baada ya takribani miaka 100 au kabla ya karne ya 16 Wareno waliichukua Zanzibar. Wareno hawakukaa muda mrefu sana na mwaka 1699 walipinduliwa na waarabu wa Oman waliorudi kuitawala Zanzibar. Kwa hiyo katika karne ya 18 Sultan wa Oman aliimarisha utawala wa waarabu katika mwambao wa Afrika Mashariki na kuufanya uwe sehemu ya Zanzibar.
Mwaka 1840 wakati Sultan Seyyid bin
Sultan alipohamisha mji wake mkuu kutoka Oman kuja Zanzibar, biashara ya
utumwa na pembe za ndovu ilistawi. Mwaka 1861 utawala wa Sultan wa
Zanzibar na Oman ulitengana baada ya kifo cha Seyyid. Katika karne ya 19
wazungu walianza kuvumbua bara, wakafuatiliwa kwa karibu na
wamishionari wa kikristo. Mwaka 1884 German Colonization Society ilianza
kutoa ardhi bara kwa kuipinga Zanzibar na mwaka 1890 Uingereza
ilichukua hadhi ya kuilinda Zanzibar, ikakomesha biashara ya utumwa na
kutambua madai ya Ujerumani kwa bara. German East Africa ilianzishwa
rasmi kama koloni mwa 1897.
Mwaka 1905-1907 Vita ya Majimaji
ilizimwa kikatili na majeshi ya kijerumani. Matukio ya duniani
yakajitokeza kwa kutokea Vita vya Kwanza vya Dunia, na kama ilivyokuwa
huko Ulaya, German East Africa haikukwepa vita hivyo, ingawa vita vikali
havikuchukua muda mrefu kutokana na kushindwa kwa German East Africa na
Waingereza 1916. Mwaka 1919 iliyokuwa Umoja wa Mataifa ndio iliipa
Uingereza mamlaka kutawala sehemu ya German East Africa aliyojulikana
kama Tanganyika. Mwaka 1946 Tanganyika ilikuwa nchi iliyo chini ya
udhamini wa Umoja wa Mataifa.
Baraza la kutunga sheria liliundwa mwaka
1926, likaongezwa mwaka 1945 na kuundwa upya mwaka 1955 na kutoa
uwakilishi sawa kwa waafrika, waasia na wazungu, kuwa na viti 30 vya
wasio rasmi na 31 walio rasmi. Mwaka 1954 Mwalimu Julius Nyerere
alianzisha chama cha Tanganyika African National Union (TANU)
kilichohimiza utaifa wa waafrika na kuleta mabadiliko ya katiba ya
kuongeza sauti ya waafrika na kutenga viti kwa ajili ya jumuiya
ndogondogo.
Uchaguzi ulifanyika mwaka 1958 na 1960.
Matokeo ni ushindi mkubwa kwa TANU ambayo wakati huo ilikuwa ikifanya
kampeni kubwa kwa ajili ya uhuru pamoja na utawala wa wengi. Serikali
mpya na serikali ya Uingereza walikubaliana katika mkutano wa katiba
mjini Uingereza kuipa Tanganyika uhuru kamili Desemba 1961. Zanzibar
ilipata uhuru 1963 kama nchi ya pekee na dola chini ya Sultan al-Busaidy
.
Tanganyika imekuwa Jamhuri Desemba 1962
mwaka mmoja baada ya kupata uhuru na uchaguzi wa urais uliofanyika
ilimwezesha kiongozi wa TANU Mwl. Julius Nyerere kuwa rais. Mwaka 1965
katiba ilibadilishwa na kuanzisha mfumo wa chama kimoja. Wakati huohuo
huko Zanzibar mapinduzi yaliyofanyika Januari 12, 1964 yalimwangusha
Sultan. Mwezi mmoja baada ya uhuru katiba ilisitishwa; Abedi Amani
Karume alitangazwa kuwa rais wa kwanza wa kiafrika wa Jamhuri ya Watu wa
Zanzibar na nchi ikawa ya chama kimoja cha Afro-Shirazi Party.
Tarehe 26 April 1964 Tanganyika na
Zanzibar ziliungana na kuunda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwl
Julius Nyerere akiwa rais na mkuu wa dola na Karume akawa makamu wa rais
na wakati huohuo akiwa rais wa Zanzibar. Mwaka 1971 Karume aliuawa huko
Zanzibar na Aboud Jumbe alichaguliwa badala yake kuwa rais wa Zanzibar
na makamu wa rais wa Tanzania. Muungano huo wa kisiasa kati ya Zanzibar
na Tanzania Bara umedumu kwa zaidi ya miongo mine ya mabadiliko.
Zanzibar ina bunge na rais wake.
Katika jitihada ya kujenga usawa katika
jamii na maendeleo ya haraka Tanzania ilianzisha ujamaa wa kiafrika.
Ujamaa, (ina maana kuwa pamoja) ulizinduliwa mwaka 1967 kwa tamko la
Azimio la Arusha na utaifishaji wa mabenki, shughuli za fedha, viwanda,
biashara kubwa, masoko kuendeshwa na bodi na wakulima kuishi katika
vijiji vya ujamaa vilivyotengwa kutoka mashamba makubwa. Mwaka 1977
vyama viwili tawala - TANU na AFRO SHIRAZI PARTY viliungana na kuunda
Chama cha Mapinduzi(CCM).
Tanzania ilirudisha mfumo wa vyama vingi
mwaka 1992 na uchaguzi wake wa kwanza wa vyama vingi ulifanyika mwaka
1995 na Chama Cha Mapinduzi kilishinda na kinaendelea kutawala kutokana
na kushinda chaguzi mfululizo.
0 comments:
Post a Comment