Comments

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ ameapishwa.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein amemuapisha Radhia Rashid Haroub kuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ.
Hafla ya kumuapisha Katibu Mkuu huyo ilifanyika Ikulu Mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Miongoni mwa viongozi hao ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi, Spika wa Baraza la Wawakilishi Mheshimiwa Zubeir Ali Maulid, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Issa Haji Gavu, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Mheshimiwa Haji Omar Kheir.
Wengine ni Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mheshimiwa Said Hassan Said, Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee, Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Hassan Othman Ngwali, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mheshimiwa Abdalla Mwinyi Khamis, Meya wa Manispaa ya Mji wa Zanzibar Mheshimiwa Khatib Abrahman Khatib, Wakuu wa Vikosi vya SMZ, Washauri wa Rais wa Zanzibar na viongozi wengine wa Serikali.
Share on Google Plus

About MZM

0 comments:

Post a Comment