MTUNZI; Moringe Jonas Mhagama
MAWASILIANO; jonasymoringe@gmail.com
MWANZO HADI MWISHO
|
Nilishuka
garini nikiwa na furaha,hii baada ya kutoka likizo baada ya miezi sita
ya kukaa chuoni.Mtu wa kwanza kumuoana alikuwa ni mama yangu ambaye
alikuwa amemshika mkono mdogo wangu ambaye alikuwa darasa la
kwanza.Nilimkumbatia mamangu huku nikiwa siamini kwani safari ya kutoka
moshi hadi Ludewa ni safari ichoshayo na yenye misukosuko mingi
sana.Baada ya kumwachia mama nilimbeba mdogo wangu ambaye baada ya
kunisalimia aliniuliza kama nitamsimulia hadithi tena nilimjibu kuwa
atasimuliwa na mama kwani nilibeba kitabu cha hadithi.Tulitoka huku
nikimuuliza mama juu ya jamaa zangu niliokuwa ni lazima niwaulizie kila
nifikapo.Tulifika nyumbani ambapo baada ya kusalimiana na babu na bibi
nioga wakati huo mama alikuwa ananiandalia chakula, baada ya kula
chakula ambacho nilikiona kitamu sana asikuambie mtu chakula cha mama
kilivyokitamu we acha tu(mola wapokee waliotangulia mbele ya haki).
Baada ya kula chakula kile ambacho nilionekana kukitamani kwa muda mrefu ,ugali wa mhogo na
samaki wa kuchomwa ,nilikaa na mama yangu tukiongea hili na lile kwani alitaka kujua mengi kuhusu safari yangu na maendeleo ya shule.Nikweli alijivunia kwani nilikuwa ni mwanaye wa kwanza wa kiume na pekee aliyefikia Chuo kikuu na mwanaye wa mwisho alikuwa darasa la kwanza.
Nyumba ilikuwa na ukimya sana baada ya yote yaliyotokea kwenye SIRI YENYE MATESO kiukweli hatukuwa na marafiki wengi wa familia kama pale kale, mama alitumia muda huo kunieleza yaliyotokea nilivyokuwa shuleni na alinitaka nikazane na nijitume kwani aliamini hakuwa na ndugu mwingine zaidi ya sisi wanawe kwani babu alikuwa ni mzee sana na muda wowote tungemzika kwani tayari alifikisha miaka tisini na nane.Nilijikuta natokwa na machozi kwani mdogo wangu alikuwa akisikiliza maneno yale kwa umakini huku akionesha masikitiko makubwa licha ya umri wake kuwa mdogo mambo yaliyoikuta familia yetu yalimfanya kuelewa vitu vingi juu ya ulimwengu huu usokuwa na hatia zaidi ya kuwabeba watu wasio na utu kabisa.
Nilikumbuka kuwa nilikuja na vijizawadi kadhaa niliamua nimtolee mdogo wangu na mama kwani nilijua waliamini mimi ndiye furaha iliyobaki kwao na mategemeo makubwa yalikuwa kwangu.Mama alinishukuru sana nilipompa kitabu cha hadithi kwani alikuwa mpenzi sana wa kusoma simulizi mbalimbali.Mara nyingi baada ya chakula cha mchana alikuwa akimsomea mdogo wangu simulizi mbalimbali za magazetini na vitabuni yote ni kuleta furaha iliyopotea kwani walionekana kukosa marafiki wengi kama awali na waliokuja pale ni kwa ajili tuu ya kuwachunguza ili kupeleka maneno kwenye vilinge vya majungu na utetaji.Japokuwa nilimpa simu nzuri yenye uwezo wa kuonesha video za mitandaoni na kupiga mziki ambayo nilinunua baada ya kubana fedha ya bodi tupewazo chuoni alionekana kukifurahia sana kitabu kile .

‘’Cha Shigongo tena ama Hussein Tuwa?’’aliuliza akicheka
‘’Hicho hata mwandishi simjui’’nilijibu nikicheka
‘’Sasa hata mwandishi humjui , umekiokota umenunua?’’ aliuliza mama akikigeuza geuza kitabu kile
‘’We unataka mwandishi au hadithi?’’ niliuliza nikichekacheka
‘’Majibu yako ya mkato kama babako’’ aliongea mama,
‘’Halafu
kaka anafanana na baba’’aliongea mdogo wangu na kwenda kukaa kwenye
kochi alilopenda kukaa baba enzi za uhai wake, na kuanza kumwigiza
akitufanya wote kucheka.Kiukweli licha ya kuwa wachache tuliotengwa na
jamii ile ilikuwa tukikutana lazima furaha ipatikane.
‘’Sasa kaka utatusomea au unataka uende uwanjani kama kawaida yako?’’ aliongea mdogo wangu
‘’Hapana sitoenda uwanjani na sasa sitocheza tena mpira ‘’nilimjibu nikionesha kusikitika
‘’Kwa
nini tena mwanangu?’’ aliongea mama akionekana kushtuka kwani nilikuwa
miongoni mwa magolikipa waliotegemewa sana pale kijijini.
‘Ngoja na wengine wacheze sahizi sie maveterani wacha tustaafu’’ niliongea nikilazimisha tabasamu usoni pangu
‘’
Wanadamu wasikukatishe mwanangu ,,,,,,,’’ kabla hajamaliza kuna mtu
alibisha hodi, alikuwa Yusuph rafiki yangu ambaye kila asikiapo nimefika
kutoka shuleni lazima aje ,aliona ni zaidi ya rafiki licha ya watu
wengi kuitenga familia yetu aliendeleza mahusiano yake mazuri kwetu
ilifika kipindi hadi alikosana na wazazi wake kwa sababu yetu.
Baada ya salamu na maswali ya hapa na pale mama alimweleza Yusuph juu ya uamuzi wangu wa kuacha kucheza mpira , naye alishangazwa sana na taarifa ile kwani alikuja na taarifa ya kunijumuisha kwenye usajili wa timu yetu ya mtaa kwa ajili ya ligi ya ng’ombe ambayo iliandaliwa na diwani wa kata ile.
Nilimwomba alitoe tuu jina langu na nafasi hiyo wapewe vijana wengine wenye uwezo wa kudaka pale mtaani huku nikipendekeza baadhi ya vijana ambao niliona wanafuata nyayo zangu.Sikuwaambia sababu kuu iliyonifanya niaachane na soka zaidi ya kumtaka mama atusomee kitabu kile nilichompa kwani hata nami sikukisoma ,nilisema hivyo huku nikijua miongoni mwa sababu zilizoufanya urafiki wetu na Yusuph ulitokana na wote kupenda sana hadithi.

Mdogo wangu ambaye alikuwa anafanya vitu vingine alisogea karibu na mama huku akisubiri mama aanze kusoma hadithi ile.
‘’Mimi
macho yananisumbua soma basi Yusuph’’alisema mama huku akimpa kitabu
Yusuph, jambo ambalo lilimfanya mdogo wangu ahamie kwa Yusuph na
kumwegamia hali iliyofanya wote kucheka kwani alionekana kutaka kukaa na
msomaji kwani mwanzoni tulidhani alitaka tuu kudeka kwa mamake hasa
kama kuna sehemu za hadithi zitatisha kumbe sivyo hivyo.Yusuph alianza
kwa kukohoa na kusoma kitabu kile akiruka kusoma utangulizi wake jambo
ambalo ndilo nililolitaka.Hadithi ilichukua zaidi ya masaa mawili ambapo
ilikuwa imewateka wasilikizaji wake, hasa na sauti ya msomaji ambayo
ilikuwa ikichukua uhalisia wa matukio kuwafanya wasikilizaji kujiona
wanashuhudia visa vilivyokuwemo hadithini. Mama alishtuka baada ya
kuangalia nje ambako aliona jua limeenda sana na kagiza kameanza kuingia
‘’Me subiri kwanza nikapike ‘’aliongea huku akisimama kuelekea jikoni
‘’Mama mi sitaki chakula’’, alisema mdogo wangu huku akimweleza kwa ishara Yusuph aendelee kusoma hadithi
‘’Kama we hutaki wenzako wasile kwa ajili yako?, ngoja nikawapikie kaka zako’’ alisema huku akiwasha taa za pale sebuleni
‘’Kaka
Moringe si alisema hali jioni’’ aliongea mdogo wangu ambaye hakutaka
hadithi ikatwe muda ule akiamini usiku atakuwa amelala hivyo kuikosa
sehemu ya hadithi ile
‘’ We
umemwona Moringe tuu , kakako Yusuph unadhani anatumia mafuta kusoma
lazima aongeze nguvu’’ aliongeza mama akitufanya wote tucheke
‘’Mama
mimi viazi nilivyokula vimenitosha kabisa labda upike kwa ajili yako’’
alisema Yusuph hali iliyomfanya mdogo wangu afurahi na kuachia tabasamu
‘’
Jamani wote mnakataa kula kisa hiyo hadithi yenu?, ngoja nijichemshie
chai hapa kuna viazi vingi tuu vimebaki najua watu fulani fulani
wanakataa kula baadaye watadai viazi.’’ Aliongea mama akinisema mimi
kwani nilivipenda sana viazi vitamu ,kama mtu akiambiwa aniue kwa sumu
aweke tuu humo lazima nitanaswa
‘’Ngoja niende mama nikachemshe hiyo chai nyie endeleeni tu na hadithi yenu’’ niliongea nikiinuka kuelekea jikoni
‘’Ukija
maswali yako mmeishia wapi hatutaki’’alinitania Yusuph na kushika vyema
kitabu na kukisoma.Nilitoka na kwenda jikoni nilipokuwa nachukua kuni
niliteleza na kutoa kilio ambacho kilisikika ndani na kuwafanya wote
watoke nje na kuuliza kilichonipata.Walinikuta nipo chini huku
nikilalamika kwa maumivu ya mguu.Mama alipandisha suruali yangu na
alichokiona mguuni kilimfanya atoe machozi hali iliyomfanya hata mdogo
wangu kulia licha ya kuwa hakuona chochote ila kilio cha mamangu
kilimfanya naye alie..
Chuma
kilichoshikilia mguu wangu ambao kiukweli haukuwa na thamani kama awali
ambayo wengi waliamini ndiyo mtaji wangu kwa kucheza soka.
''Mwanangu
nini hiki?''Aliuliza mama huku machozi yakizidi kumtoka sauti yake
ilizidi kunipa uchungu nikijuta kumficha.Sikutaka kumuumiza mama yangu
kwa taarifa yangu na mazoea yangu ya kwenda bafuni nikiwa nimevaa
suruali na taulo begani nilijua ingeficha siri yangu.
''Nilipata
ajali mama''Niliongea kwa sauti ya kinyonge ambayo nayo ilikuwa na
chechembe za uchungu,wakati huo Yusuph alikuwa akiniangalia kwa uchungu
mkubwa alijua kabisa isingekuwa vyema kuongeza machungu kwa mama na
mwana waliokuwa pale chini.
''Ajali gani mwanangu?''Mama alizidi kuongea kwa sauti ya uchungu huku mdogo wangu akiwa anatuangalia huku machozi yakimtoka.
''Tulipata
ajali safarini chuoni''Nilimjibu huku nikijaribu kuinuka nikisaidiwa na
Yusuph ambaye alikuja kuniinua na kuelekea ndani.Nilisikia maumivu
fulani ya mfupa lakini niliamua kujikaza kwani nilijua kulalamika zaidi
kungemuumiza zaidi mama jambo ambalo sikutaka kuliruhusu litokee.
''Msihuzunike
sahizi nimepona na nimeshazoea''Niliongea na kulazimisha tabasamu
ambalo sikujua kama lilionekana kama ni la ukweli mbele ya waliokuwa
wakinitazama.
''Kumbe
hujapenda mwenyewe kuacha mpira bali shida tuu
zimekulazimisha?''Aliongea mama kwa uchungu mkubwa kwani mara nyingi
nilimwambia lazima mpira uje kubadilisha maisha yetu sasa mguu
haukuniruhusu tena kutimiza ndoto zangu nilizokuwa naziota tangu nikiwa
mdogo.Nilikumbuka kipindi kile nachaguliwa kuwa golikipa bora wa kila
mashindano huku uhodari wangu wa kudaka penati ukizidi kunifanya niwe
naaminiwa na kila mtu kwenye timu mara itokeapo penati,hali iliyowafanya
hata wachezaji kuwa tayari kucheza rafu kwenye eneo hatari maksudi
wakimwamini mtu ambaye alienda kupigiwa penati hiyo.
Katika maisha yangu ya soka niliwahi kufungwa penati mbili tuu tena siku ya fainali ya mashindano fulani lakini siku ile nilidaka tatu hicho ndicho kilichomfanya kila mtu aamini kitu kitakachonipa pesa na umaarufu ni soka na si kingine na hata shuleni nilikokuwa naenda nilienda nikiamini kupitia huko ningeweza kupata timu lakini hata kabla ya kujiunga na timu ya daraja la kwanza ambayo ilikuwa Mjini Moshi nilikuwa nimepatwa na kitu kilichozima ndoto zangu.Licha ya timu ile kunitaka niitumikie huku nikiwa chuoni nilikataa na kuwataka wanitumie kipindi cha likizo ama nikimaliza jambo ambalo walikubaliana nalo huku nikishiriki kwenye michezo ya kirafiki iliyofanyika mwisho wa wiki.

Ajali
ilizima ndoto zangu jambo ambalo lilinifanya nitafute kitu kingine cha
kufanya ili kuboresha maisha yetu na kuwapa mama na mdogo wangu furaha
ya kweli.Niliamua kuandika vitabu vya hadithi kwa msaada wa marafiki
zangu wakubwa Tumsifu Joo-Chan Kaoza, Nyemo Chilongani,Yustina
Emilian,Hilda Kigola,Tamasha Paulo na wengineo wengi ambao waliamua
kunisaidia kutimiza lengo langu.Kitabu cha kwanza ndicho kilichikisomwa
wakati ule nikiamini itakuwa ni sehemu ya furaha ya familia ile
iliyobakiwa na upweke wa ajabu usioelezeka.
''Tuendelee
na simulizi mama haya mengi yapo yataisha tuu siku moja'Niliongea
nikimtaka Yusuph asome kitabu kile lakini alionekana kuwa mwenyeengi
pelekea kumnyang'anya kitabu kile na kukisoma kwa sauti ila na hisia za
hali ya juu .
''SHUKRANI ZANGU PIA KWA MAMA YANGU MZAZI Kalista Haule na mdogo wangu mpenzi kwa kuwa sehemu ya furaha maishani mwangu.
''MUNGU HUWEKA NJIA NAJUA NDOTO ZANGU ZA KUSAIDIA FAMILIA YANGU ZITATIMIA’’.
Asanteni sana .
Moringe Jonas Mhagama.
Ilisomeka
sehemu ya mwisho ya utangulizii wa hadithi ile ambayo iliwafanya
waliokuwa wakinisikiliza wacheke na kuninyag'anya kitabu kuona kama
yaliikuwa ya kweli.
''Kweli!''
aliongea mama kwa mshtuko mkubwa na kuja kunikumbatia akitoa machozi
,machozi ambayo kwa wakati huu yalikuwa ya furaha si kama awali alipoona
chuma mguu mwangu.
''Mwanangu mshukuru Mungu kwa vipaji alivyokupa ulishindwa amekuleta huku''Aliongea mamsauti ambay kama ya kilio ama kicheko.
''Umezoea
kuona machozi yangu mwanangu,lakini chozi hili ni tofauti na machozi
mengine hili ni CHOZI LA FURAHA MWANANGU''Aliongea kucheka kwa sauti
iliyowafanya hata Yusuph na mdogo wangu wacheke na kunipongeza.
MWISHO............
0 comments:
Post a Comment